Shirika lisilo la Kiserikali la Pastoralist Women Council linalofanya kazi zake katika Wilaya tatu za Monduli, Longido na Ngorongoro Mkoani Arusha limeendelea kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kumtua mwanamke ndoo kichwani, kwa kujenga miundombinu ya Maji itakayoiwezesha Jamii ya kifugaji ya Monduli kupata Maji ya kutosha kwa matumizi ya nyumbani na mifugo pia.
Akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika Kata ya Esilalei na Engaruka Mhe. Festo Shem Kiswaga Mkuu wa Wilaya ya Monduli amelipongeza Shirika hilo la PWC kwa kuichagua Monduli kuwa Moja ya Wilaya tatu za kunufaika na mradi huo wa Maji.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo Bi. Nalemuta Ndonyo Mratibu wa haki na Uongozi wa Shirika hilo la PWC amesema Mradi huu wa MajiUnagharimu jumla ya shilingi milioni 580 ambapo Serikali kupitia RUWASA wameongeza jumla ya shilingi milioni 100 ili kuhakikisha Mradi unakamilika kwa wakati.
Ameongeza kusema kuwa Shirika limetoa jumla ya tank za Maji 50 za Lita 5000 kwa ajili ya kuhifadhi Maji, wamejenga majiko 50 ya kupikia, wametoa mafunzo ya ufundi (cherehani na umeme) kwa vijana19 na vijana wengine 20 wako shule pamoja na kutoa jumla ya mbuzi 273 kwa Wanawake 85 ili kuwawezesha kukua. kiuchumi
Kwa upande wake Eng. Msaki kutoka RUWASA Monduli amethibitisha Serikali kuchangia milioni 100 katika mradi huo lakini pia kufanya utafiti wa maeneo rasmi ya kuweka vyanzo vya mradi huo.
Mhe. Kiswaga amehitimisha kwa kuwataka wananchi kuzipokea NGO'S kama PWC zenye lengo zuri la kuboresha maisha ya Watanzania huku akikemea viongozi na wananchi wote wanaochochea Jamii kupinga suala la uwekezaji.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli