Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha imeadhimisha Siku ya kisukari Duniani Novemba 15, 2024 katika Viwanja vya Polisi Kata ya Mto wa Mbu, Kwa kutoa Elimu ya lishe inayozingatia muongozo wa sasa wa Kitaifa wa ulaji wa chakula bora na mlo kamili ili kuepuka uzito mkubwa unaopelekea magojwa kama kisukari na shinikizo la damu.
Akizungumza, Bi. Havijawa Salim Mgeni wa Heshima katika Maadhimisho hayo ambaye pia ni Katibu Tarafa wa Tarafa ya Mto wa Mbu, amewataka Wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara huku akiishauri jamii kuacha kuwanyanyapaa watu wenye changamoto ya magonjwa hayo ya kisukari.
Naye Bi. Adventina Nyambuya Afisa Lishe kituo cha Afya Mto wa Mbu ambaye pia ni Mmoja wa Wana Club ya Lishe wanaohudumia watoto wadogo wenye changamoto ya kisukari, amewataka Wananchi na Wafanyakazi kujikita katika kufanya mazoezi ya mwili ili kupunguza ama kuondoa mazingira ya mwili kupata magonjwa kama kisukari, na shinikizo la damu.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli