MKUU WA WILAYA YA MONDULI AKABIDHI GARI YA DHARURA (AMBULANCE) HOSIPITALI YA WILAYA YA MONDULI.
Akizunguzungumza na wananchi pamoja na Wauguzi Hospitalini. Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Joshua Nassari amesema kwamba kama kuna sekta ambazo zimeguswa kupitia serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dtk Samia Suluhu Hassan kwa kipindi kifupi kwamaana ya miundo mbinu ya majengo,vifaa tiba,miundo mbinu ya vyombo vifaa vya usafiri,wataalamu kuongezwa ni sekta ya afya.
"Namuaidi Mh.Rais DKt.Samia Suluhu Hassan kwamba tutalinda fedha na vifaa tulivyoletewa kwa umakini na niombe tu Mwenyekiti kwamba wasipewe madereva ambao hawana uzoeefu ili kutunza rasilimali zetu" 'Amesema Nassari'
Kwa upande wake Dkt Lengai Edward Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli amesema kwa upande wa sekta ya afya mpaka sasa tumeshapokea magari mawili kwa kipidi kifupi kwanza mwezi uliopita mwezi wa 12 Disemba tumepokea gari aina ya (toyota land cruser) kwaajili ya usimamizi shirikishi kwani imekuwa msaada kuvifia vituo.Na gari nyingine ni (ambulanca) gari ya dharura ambapo gari hii itakwenda kuwezesha huduma ya dharura kwa wagojwa.
Queen Fred ni Mkazi wa Monduli mjini amemshukuru Dkt Samia Suluhu Hassani Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzani kwa kuwaletea gari ya dharura yaani (ambulance) kwani litasaidia kuokoa maisha ya wananchi wengi lipohitajika kutumika kwa haraka.
"Rai yangu kwa watumishi wa afya kazi zinazofaywa na serikali tunataka tuzione pia kwenye utoaji huduma za afya.tuwe na moyo wakuhudumia wagojwa mahospitalini lakini pia kujituma kwa bidii."amesema Nassari.
Imeandaliwa na :
Kitengo cha mawasiliano serekalini
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli