Akizungumza na wananchi wa kata ya makuyuni amewahakikishia wananchi hao kwamba kero zao zitatuliwa nakusikilizwa napia utekelezaji wa utatuzi wa kero zao kwa haraka.
Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha Oldonyo bwan.KERIKA MATUNI MOLLEL ameeleza kero yake mbele ya mhe.mkuu wa wilaya kero hiyo inayohusu ardhi eneo la malisho ya mifugo.kwani wamekuwa wakipata tabu na askari kuwasumbua kupisha eneo hilo.ambapo kaimu mkurugenzi Bi.Rose Mhina amemueleza kuwa kwa kuwa afisa ardhi yupo hapa kero yako itatatuliwa.
Sambamba na hilo mkuu wa kitengo cha afya amewaeleza wanchi wa kata ya Makuyuni kuwa serikali ya awamu ya sita kupitia ofisi ya Tamisemi wamepokea taarifa kwamba ifikapo mwaka 2024/2025 mwaka mpya wafedha sehemu iliyobakia ya ujenzi wa jengo hilo la kituo cha afya utakamilishwa.
Hatua hivyo wakazi wa Makuyuni wakiwakilisha kero ya swala la umeme wa rea kufika vijijini...Mhandisi wa wilaya bwan. yusuph Mchoro awajibu mpaka kufikia mwezi wa kumi mbili tiari vijiji vyote vimeshaandikiwa hivyo mwaka mpya wa fedha mwezi wa saba mwakani umeme utawaka vijijini.
Akihitimisha mkuu wa wilaya ya monduli mhe.Joshua nassari amewataka wakazi wa kijiji cha Moita kutulia kwa utulivu kwani yeye pamoja na kamati ya usalama watakwenda kutembelea eneo la ardhi Moita nakuitatua kero yao.pia ameshukuru serikali ya awamu ya sita chini ya rais SAMIA SULUHU HASSANI kwa kuwaletea fedha kwa ajili ya maendeleo hasa katika sekta ya afya na elimu.n.k.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli