Mitungi hamsini (50) ya Nishati safi (Gesi) imetolewa bure kwa Mama lishe na Baba lishe Wilaya ya Monduli, ikiwa ni moja ya mkakati Kabambe wa mapinduzi ya matumizi ya nishati isiyo safi yaani mkaa na kuni iliyokuwa ikitumiwa na Watanzania walio wengi.
Mpango mkakati huu ulioanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan una lenga kuboresha maisha ya watanzania kwa kuwafanya waondakane na matumizi ya nishati isiyo safi ya kuni na mkaa ambayo kwa namna nyingine imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa Mazingira kwa kukata miti hovyo ili kuchoma mkaa.
Akizungumza wakati wa zoezi la ugawaji wa mitungi hiyo ya gesi Mhe. Festo Shem Kiswaga amesema " Huyu Mama anataka atuondoe kwenye umaskini; Ukiona Kiongozi mkubwa wa nchi katika hotuba zake anazungumzia suala la kuondoa matatizo na changamoto kwa watu wa chini basi ujuwe huyo ni kiongozi." Sasa 'Tuseme Moshi basi' . amesema Mhe. Kiswaga
Naye Ndg. Isack J. Copriano Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo amesema kuwa Rais Samia ameendelea kuwa Rais wa mfano katika nchi yetu hivyo tuendelee kumuombea Mhe. Rais kwa jinsi anavyo wajali Watanzania na Wana monduli.
Kwa upande wake Dkt. George Kasibante kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness R. Laizer, amesema " Tunatambua kazi mnayoifanyo huko ya kuhakikisha Watanzania wanashiba na wanafanya kazi ya kuzalisha uchumi, na Mama Mhe. Samia ameona atoe majiko ili mpunguze kutumia kuni na mkaa. Amesema Dkt. Kasibante
Naye Ndg. Paulo Mollel Baba Lishe na Mkazi wa Mswakini Wilayani humo amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia nishati hiyo ya kupikia ambayo itawapunguzia adha ya kutafuta kuni na mkaa na hata kuboresha biashara zao huku akisema " Mama mitano Tena".
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli