Mkurugenzi mtendaji (w) Monduli Ndg. Anderson S. Ulaya amepokea taarifa za kujiuzulu kwa madiwani sita(6) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Madiwani waliojiuzulu ni Loth Mollel kata ya Meserani, Solomon K mollel kata ya Lolkisale, bariki Sumuni kata ya Monduli juu, Edward lenanu kata ya Naalarami, Benedict Mawala kata ya migungani na Einoth Leenga viti maalumu.
Kwa mantiki hii idadi ya madiwani waliohamia CCM kutoka CHADEMA imefika saba ukiongeza diwani mmoja wa kata ya moita Edward Sapunyu aliyejiuzulu mwishoni mwa mwaka jana.
Mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 CHADEMA kilipata nafasi nyingi za udiwani ukilinganisha na CCM, CHADEMA ilipata viti 18 na CCM viti 9 lakini madiwni wa CHADEMA wameendelea kutimkia CCM siku kwa siku.
Mhe. Julius kalanga ambaye ni mbunge wa jimbo la Monduli (CHADEMA) katika ukurasa wake wa facebook amekiri kupata taarifa za kujiuzulu madiwani hao. Amesema kuwa chama kimepata pengo kwa madiwani hao kujiuzulu lakini anaheshimu uamuzi wao wa kikatiba na anawatakia kila la heri huko waendako.
Imeandikwa na E.Msifuni
Afisa TEHAMA (W)
MONDULI.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli