Mbunge wa jimbo la monduli Mhe. Fredric Lowassa amegawa Vifaa vya TEHAMA ikiwemo Computer na Projector kwa shule nne za msingi za wilaya hiyo ambapo ni utekelezaji wa ahadi yake aliyo iahidi wakati wa mashindano maalum ya kimichezo kwa shule za msingi yaliyofanyika mwaka jana na kuhusisha shule za msingi wilaya ya Monduli, ambapo mmbunge alihidi zawadi kwa mshindi pamoja na shule tatu za pembezoni.
Mhe. lowassa amesema utekelezaji wa ahadi hiyo ni sehemu ya kuboresha elimu kupitia michezo katika wilaya hiyo, huku akikiri kuwa amepokea taarifa ya mabadiliko mazuri ya kitaaluma baada ya mashindano hayo, na kuahidi kuendelea kutoa motisha zaidi.
katika zoezi hilo la ugawaji wa vifaa hivyo pia limehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe Joshua Nasary ambapo amempongeza mbunge Fredric kwa motisha hiyo anayo itoa huku akiwahasa waalimu kutumia vifaa hivyo kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo badala ya Nadharia pekee.
Mhe Nasari Amemhasa mbunge kuendelea kutoa motisha hiyo kwa shule zingine za wilaya ili kuboresha uwezo wa wanafunzi katika sayansi na Teknolojia ambayo imeongeza kiu ulimweni.
Mwalimu Prosista Shayo ni afisa elimu taaluma Wilaya ya Monduli kwa shule za msingi amesemea idara ya Elimu inamshukuru mbunge lowassa kwa utekelezaji wa ahadi iyo kwani michezo na elimu ni kitu kimoja na michezo inasaidia kukukuza taaluma zaidi.
kwa upande wake Mwalimu Richard Ngoda ambae ni afisa michezo na tamaduni wilaya ya Monduli amesema kwa juhudi hizo za Mhe lowassa zitasaidia kuiongezea michezo dhamani na kuchochea mwamko kwa shule zile zilizo puuza dhana ya michezo.
huku waalimu wa shule zilizopokea zawadi nao wakishukuru kwa mkono huo wa ahsante wa mhe mbunge.
Zawadi hizo za vifaa vya tehama imetolewa kwa shule nne za msingi wilaya ya Monduli ambayo ni Losingirai, lesimingori, loksale na shule ya msingi manyara ranch
licha ya kwamba mashindano hayo yalihusisha shule za kata zote ndani ya wilaya ya Monduli ambapo kwa kila kata pia walifanikiwa kupokea zawadi ya jezi kwa washindi wa ngazi ya kata. katika mashindano hayo Shule ya msingi manyara rench iliibuka kidedea.
Na Obed Emmanuel
Ofisi ya TEHAMA
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli