Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amesema kamwe hatoacha kuwawajibisha wazembe, wavivu na watendaji wote wa Mkoa wa Arusha wasiotimiza majukumu yao kikamilifu licha ya kuongezeka kwa kelele na ukosoaji unaoelekezwa kwake kutokana na mtindo wake wa Uongozi.
Mhe. Paul Christian Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Mei 27, 2024 wakati akizungumza na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli ikiwa ni siku yake ya tatu ya ziara za kutembelea wilaya zote za Mkoa wa Arusha ili kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kauli ya Mhe. Mkuu wa Mkoa imekuja kufuatia baadhi ya watu kunukuliwa na vyombo vya habari wakimtaja Mhe.Makonda kama mdhalilishaji wa watumishi wa Umma ndani ya Mkoa wa Arusha, suala ambalo Mkuu wa Mkoa amelitaja kutombabaisha ama kumpunguzia kasi katika kusimamia watendaji wavivu na wazembe wanaoshindwa kutimiza majukumu yao katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli