Katibu Tawala Wilaya ya Monduli (DAS) Ndg. Muhsin Kassim leo Oktoba 26, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli amefungua mafunzo ya siku moja(1) kwa vyama vya Siasa Wilaya ya Monduli yenye lengo la kutoa elimu kwa UMMA kuhusu Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akifungua mafunzo hayo Ndg. Muhsin kassim amewataka wajumbe wa mafunzo hayo kuwa makini na wasikivu wakati wote wa mafunzo, ili waelewe vema yote yanayofundishwa na wanapo maliza mafunzo hayo wakawe mabarozi wema kwa kutoa elimu hiyo kwa wananchi bila kujali aina za vyama vyao kwa kuwa Amani ya nchi ni tunu na faida kwa wananchi wote wa Tanzania.
Aidha, Ndg. Muhsin Kassim amewaeleza wajumbe hao kutoka vyama vya Siasa Wilaya ya Monduli kuwa anaamini Uchaguzi huu utakuwa wa haki na Amani kwani Serikali kupitia vyombo vya usalama imejipanga na inaendelea kusimamia vema hali ya utulivu na amani.
Naye mtoa mafunzo hayo Ndg. Emmanuel David Msengi Afisa kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa Nchini amewaeleza wajumbe hao kutoka vyama vya Siasa Wilaya ya Monduli utoaji elimu ya uraia kwa vyama vya Siasa na demokrasia, huku akiwataka kuzingatia Sheria, kanuni na maadili ya vyama vya siasa katika kuratibu mikutano ya hadhara katika kipindi hiki cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake Ndg. Remmy E. Rummas Katibu wa Chama cha Chadema Wilaya ya Monduli ameiomba Ofisi ya Msajili kusimamia watu wote wanaofanya dhihaka kwa vyama vingine kwa kushusha bendera ya vyama hivyo wakati wa kampeni na wakati wa Uchaguzi wachukuliwe hatua ilikuendelea kulinda amani na Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa uende vizuri kwakuwa Uchaguzi huu ukienda vizuri hata uchaguzi ujao utamaluzika salama.
Kwa upande wake mjumbe wa Chama cha mapinduzi (CCM) Bi.Beatrice J.Maudiya amewataka wajumbe wengine kutoka vyama vingine vya Siasa kuachana na dhana za miaka iliyopita katika Uchaguzi na kuwataka wajumbe wa vyama vyote vya Siasa kueleza sera zilizonzuri ambazo zitawavusha Watanzania katika miaka mitano ijayo na sikutoka kashfa majukwaani ili uchaguzi wa haki na amani.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli