Maadhimisho ya mtoto wa Africa wilaya ya Monduli yamefanyika kata ya Majengo tarehe 14.6.2024 ambapo maadhimisho hayo yalilenga kumuelimisha mtoto pamoja na kumlinda mtoto katika malezi bora kwa kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi.
Halmashauri ya wilaya ya Monduli imekuwa ikiratibu masuala yanayohusu watoto kwakushirikiana na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha watoto wanakuwa salama na wanapatiwa haki zao za msingi.
Kwaniaba ya mkuu wa wilaya ya Monduli katibu tawala wilaya ndug.Muhsin kassim amesema kuwa baadhi ya mila na mitindo ya maisha inamadhara na kudhalilisha utu wa mtanzania hasa mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na ukeketaji njia inayotumiwa na baadhi ya makabila ya kumvusha rika mtoto wa kike.licha ya kumdhuru mwilu,lakini inamuandaa mtoto wa kike kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na ndoa katika umri mdogo.
Amesisitiza Das wilaya kwamba,ili kuhakikisha kwamba wazazi na walezi wanatoa malezi chanya kwa watoto wetu ili wastawi na kukua vema hatuna budi kuyazingatia mambo makuu matatu,
*kumtimizia mtoto mahitaji yake ya msingi,yakijumuisha chakula chenye lishe huduma za afya,elimu na mavazi na malezi.
*mtoto alidwe dhidi ya vitendo vya ukatili.
*mawasiliano mazuri yaimarishwe kati ya mzazi na mtoto.
Sambamba na hilo katibu tawala wilaya ya monduli ametoa vyeti kama pongezi na keki ndogo kwa wadau mbalimbali na mashirika pamoja na taasisi mbalimbali zinazohudumia watoto wilaya ya Monduli na waliofanikisha maadhimisho hayo kufanyika kwa michango mbalimbali.
Maadhimisho hayo yaliyobeba kauli mbiu inayosema "Elimu jumuishi kwa watoto izingatie maarifa maadili na stadi za kazi"kauli mbiu hii iwakumbushe wazazi au walezi na jamii katika utoaji elimu inayojumuisha watoto wote,isiyobagua mtoto kutokana na hali yake,elimu itolewe Bila kujali jinsia,tabaka,umri,dini,lugha,maoni ya kisiasa,ulemavu,hali ya kiafya,ulemavu,n.k.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli