Wajumbe wa kikao Maalum cha kamati ya Afya ya msingi na harakishi wa chanjo ya UVIKO 19 Katika halmshauri ya wilaya ya Monduli wameagizwa kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa jamii kuhusu chanjo ya UVIKO 19 ili kuongeza hamasa ya kupata chanjo kwa wanchi.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe. Frenk Mwaisumbe wakati akifungua kikako hicho leo 27.09.2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya monduli ambapo amesema ili kuhakikisha wananchi wanapata mwamko wa kupata chanjo ni lazima kila mmoja awe tayari kutoa elimu popote alipo bila kujali mazingira atakayo kuwepo.
Amesema kumekuwa na maswali mengi kutoka kwa kwa wanachi juu ya chanjo hiyo ya UVIKO 19 hivyo kuna haja ya kujitolea kwa hali na mali kujibu maswali hayo ili wananchi waendelee kuongeza uelewa na kuondoa mashaka juu ya chanjo hiyo.
Amesisitiza kuwa ili kuepuka vifo vinavyo sababishwa na ugonjwa Wa huo wa UVIKO 19 ni lazima kuchukua wajibu huo wa kutoa elimu na hamasa kwa jamii kama kazi zingine za kila siku.
Naye Mganga mkuu wa Wiliaya Dkt. Lengai Edward amesema kwa takriban miezi miwili sasa tangu kuanza kutolewa chanjo ya UVIKO 19 nchini hakuna madhara yeyote ya kiafya yaliyo ripotiwa miongoni mwa walio chanjwa hali inayo thibitisha usalama wa chanjo hiyo.
Amesema hadi kufikia tarehe 26.09 2021 ndani ya wilaya ya Monduli idadi ya wananchi walio chanjwa wamefikia 1,777 sawa na 48.7% ya malengo waliyo wekewa na wizara ya afya ya kufikia watu 3,650 sawa na 100%.
Aidha amesema kwa sababu hiyo ndiyo maana serikali imeamua kuanzisha mpango shirikishi jamii na harakishi wa kuongeza kasi ya utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 Kwajili ya kufikia sehemu kubwa ya Jamii, ambapo chini ya mpango huo idadi ya vituo vya kutolea huduma vimeongezeka ambapo kwa wilaya ya monduli awali kulikua na vituo vitatu na sasa vitaongezeka hadi kufikia vitoa 22.
Lengo la kikao hicho kwanza ni kuwajengea uwezo viongozi mbali mbali wa makundi ya jamii wakiwemo viongozi wa kidini, kimila,serikali na watu mashuhuri ili kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusiana na usalama na umuhi u wa chanjo ya UVIKO 19 kwa mtu mmoja mmoja na kwa Taufa kwa Ujumla.
Pili ni kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kufikia sehemu kubwa ya jamii ya wana monduli kwa elimu na huduma ya chanjo ili kuyafikia malengo kwa asilima 100 ifikapo tarehe 14.10.2021.
Baadhi ya wajumbe walio hudhuria kikao hicho maalum wakiwemo viongozi wa dini wametoa mchango wao ambapo Askofu Mkuu wa Makanisa ya Peace Evangelical Churches Askofu Jacob Mwaigaga Amesema kuna haja ya kupita nyumba kwa nyumba kutoa Elimu hamasa kuliko kuwaita wananchi kwenye mikutano kwani watahudhuria wachache zaidi.
Naye sheak wa Msikiti wa Mto wa Mbu Sheak Nasibu Idd Nasibu amekihakikishia kikao hicho kuwa kama mwakilishi wa Viongozi wa dini atakua mstari wa mbele kutoa elimu na hamasa kwa wananchi.
Imeandikwa na Kuchapishwa na
Obed Emmanuel
Ofisi ya TEHAMA Halmashauri ya Monduli
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli