Mwenyekiti wa kamati ya Elimu,Afya na Maji Mhe.Loth Tarakwa ambaye ni Diwani wa kata ya Meserani Wilayani Monduli, leo Januari 15 ,2025 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo ameongoza kikao hicho chenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kielimu, afya na maji ili kuboresha Elimu , afya na upatikanaji wa maji Wilayani Monduli.
Akiwasilisha taarifa ya robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Bi.Magreth Muro Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Monduli amesema "viwango vya ufaulu Kwa kidato cha nne vimepanda kutoka 98% Mwaka 2023 hadi 99% Mwaka 2024 Kwa daraja la kwanza."amesema Bi.Magreth Muro
Kwa upande wake Mhe.Thomas Meiyan Diwani wa Kata ya Monduli juu, amezugumzia tatizo la mimba mashuleni Kuwa ni suala linalorudisha nyuma Upandaji wa viwango vya ufaulu huku akisisitiza wazazi wa Wanafunzi hao kuelimishwa juu ya kuwarudisha shuleni Wanafunzi waliopata changamoto ya ujauzito zaidi ameshauhauri Wanafunzi hao kupewa ushauri ili waone umuhimu wa kurudi shuleni.
Kwa upande wa Elimu Msingi Ndg. Kirusha Laizer kwaniaba ya Afisa elimu Msingi amesema suala la mimba katika shule za Msingi limepungua kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na walimu na wadau wa elimu.
Naye Dr.George Kasibante ambaye ni Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ameieleza kamati hiyo kuwa, hali ya huduma za afya katika Halmashauri hiyo imeboreshwa na huduma za afya zinatolewa vizuri kwa kuzingatia utoaji bora wa huduma (customer care) katika hospatali,zahanati na vituo vya afya.
Aidha Dr.Kasibante amesema kuwa kwa mwaka huu hadi Sasa Halmashauri imepokea watumishi wapya 79 hivyo kuongeza nguvu kazi katika sekta hiyo na kwamba , vifaa tiba na dawa vinapatikana katika hospatalizi, Zahanati na vituo vya afya sambamba na kuboresha huduma za lishe kwa watoto waliochini ya miaka miatano (5) huku miundombinu ya afya inaendelea kuboreshwa.
Akihitimisha kikao hicho Mhe.Loth amesisitiza utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa na kamati, huku akisisitiza utoaji wa elimu kwa wazazi wa wanafunzi waliopata ujauzito shuleni ili waone umuhimu wa kuwarejesha wanafunzi hao shuleni.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli