Ndg. Anael Mbise Afisa Tawala Wilaya ya Monduli kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya DCC Wilayani humo Mhe. Festo Shem Kiswaga leo Feb. 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo, ameongoza kikao cha Kamati hiyo chenye lengo la kujadili na kupitisha mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa Mwaka wa fedha 2025/2026.
Akizungumza katika kikao hicho Ndg. Anael Mbise amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa ufuatiliaji, usimamizi na kukusanya mzuri wa mapato yeye pamoja na Watendaji wake wote na kupelekea kuongezea kwa makusanyo Wilayani humo kwa ongezeko la asilimia 3.9 kutoka asilimia 3.0
Aidha, Ndg. Anael Mbise amewataka Maafisa Watendaji wote wa Kata na Vijiji kumsaidia Mkurugenzi kuhakikisha wanasimamia vizuri ulipaji wa ushuru wa Mifugo katika maeneo yao kwa kuwa kama jitihada zitaongezeka Halmashauri inaweza kuvuka kiwango cha bilioni 3.9 hadi kukamilisha bilioni 4 na hili litawezekana zaidi kwa kuziba mianya ya rushwa kwa kutoa risiti kwa kila malipo yanayofanyika.
Akiwasilisha mapendekezo ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2026 Ndg. Lucas Daud (DPLO) katika Halmashauri hiyo, amewapitisha wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya hiyo (DCC) kwenye Bajeti ya 2023/2024 kwa kueleza mafanikio, changamoto na ufumbuzi wake, sambamba na kueleza mapitio ya nusu mwaka ya Bajeti ya 2024/2025 yenye jumla ya Tsh. Bilioni 46.5
Ndg. Lucas amebainisha kuwa kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli imekusudia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi bilioni 48.1 ambayo ina ongezeko la asilimia 3.4 ukilinganisha na bilioni 46.5 kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Naye Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ametoa shukrani kwa Menejimenti, Watendaji wa Kata na Vijiji na wote wanaohusika katika ukusanyaji wa mapato kwa ushirikiano mzuri uliopelekea ufanisi katika zoezi la ukusanyaji mapato ambapo kufikia Disemba 2024 Halmashauri ilikuwa imefikia asilimia 75 ya malengo ya makusanyo.
Aidha, Bi. Happiness ameshukuru Serikali ya awamu ya 6 ya uongozi makini wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia asilimia 100 ya fedha za Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri yetu ya Monduli.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli