Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Festo Shem Kiswaga leo Aprili 4, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya hiyo amekabidhi hundi ya shilingi Milioni 589 kwa vikundi vilivyokidhi kupewa mikopo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe.Kiswaga amesema Kuwa mikopo hii Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amelenga kuinua uchumi wa Watanzania wote mijini na vijijini hivyo pesa hizi zitumike vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa,kwanamna mlivyoomba kwenye makundi yenu.*-
Akisoma taarifa ya utoaji wa mikopo Ndg.Lawi ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Jamii Wilayani Monduli amesema Kuwa jumla ya shilingi milioni 589 inayotolewa timu ya menejimenti ya kamati ya uhakiki ya Wilaya imependekeza vikundi 36 kupatiwa mikopo ambapo ni katika mchanganuo huuu, vikundi 24 vya wanawake,11 vya vijana, na kikundi kimoja cha watu wenye ulemavu.
Bi.Happiness R. Laizer ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Monduli amewapongeza wanavikundi waliyokidhi vigezo vya kupatiwa mikopo hiyo nakuwataka kutumia fedha hizo Kwa malengo yaliyowekwa na kikundi ili kuweza kufanikiwa katika biashara na kujiinua kiuchumi Kwa ujumla.
Kwa upande wake Bi. Lidya Mauki ambaye ni Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Monduli, amewapongeza wanufaika hao wa mkopo huku akiwaeleza kuwa pesa wamekopeshwa bila riba hivyo ni vyema kuwa waaminifu na kuweza kurejesha na asitokee mtu adanganye apewe fedha hizo kwani fedha hizo zimetolewa na Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Neema Kichuya,ni mnufaika wa Mkopo Kwa niaba ya wanufaika wenzake ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kuwapatia fedha za mikopo ambayo itawasaidia kiimarisha uchumi wao kwa maendeleo binafsi na Jamii Kwa ujumla.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli