Kutokana na Mvua nyingi zinazoe endelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha adha kwa wakazi wa baadhi ya maeneo ikiwemo mafuriko na uharibifu.
Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe. Fredrick Lowassa amelitembelea eneo la bonde la ufa mto wa Mbu amablo nj miongoni mwa kata zinazoiunda wilaya ya monduli na ni miongoni mwa maeneo yalio kumbwa na mafuriko kipindi hiki cha mvua ili kujionea khali ya uharibifu katika eneo hilo.
Baada ya kufika katika eneo hilo Mhe. Lowassa (mb) alizungumza na Viongozi pamoja na Wahanga wa mafuriko hayo (Wanamchi) ambapo alikiri kwamba hali ya eneo hilo airidhishi hivi sasa hivyo ameiomba Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kulitazama eneo hilo kwa jicho la Huruma na kulitafutia ufumbuzi kudumu.
Alisema eneo hilo la Mto wa Mbu limekua likikumbwa na mafuriko mara kwa mara licha ya kwamba wataalamu wamekua wakifika kufanya tadhmini baada ya mafuriko lakini mpaka hivi sasa hakujapatikana ufumbuzi wa changamoto hiyo.
Aidha Alisema ni wakati sasa wa Kuchukua uamuzi na kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo kwa wakazi wa mto wa Mbu huku akiwarai wakazi hao kuwa mstari wa mbele kuanza kufanya tathmini kwa kuandika na kuifahamu dhamani ya mto wa mbu kwani wao ndio wanao jua maeneo korofi yanayo sababisha athari.
"Kabala hatujaenda kupambana na Serikali tuyafanye yale kwanza ambayo sisi tunayamudu kwani yale ambayo tunayamudu ndio na mimi naweza kuingiza mkono Wangu kama mbunge wenu na hayo mengine lazima tuya documents kutuma Kwenye Serikali"
"Kazi hii ambayo tunaweza kuifanya wenyewe kama kufukua mitaro naomba tuanze kuifanya wenyewe kwa kuwatumia vijana wetu waanze kufanya kazi hiyo na ni lazima watambue kuwa hii ni changamoto" amesema Lowassa.
Mhe. Lowassa alisema chanzo kikubwa cha mafuriko hayo ni mito kuziba hivyo wataanza na zoezi la kusafisha mito kwa kushirkiana na Uongozi wa mkoa na kuiwasilisha taarifa bungeni ifike kwa waziri mwenye dhamana na ianze kufanyiwa kazi kwanzia mwezi July mwaka huu.
Alisema kuna haja kubwa ya Serikali kuitazama Mto wa Mbu kwasababu Eneo hilo ndilo lango kuu la mapato makubwa ya Serikali kupitia utalii kwani eneo hilo ni njia kuu inayo unganisha hifadhi za taifa ikiwemo Ngorongoro, Manyara pamoja na Serengeti ambazo ni hifadhi tajika kitaifa.
"kata ya mto wa Mbu yaani bonde hili ndilo lango kuu la mapato yote makubwa ya utalii ya Serikali ya Tanzania, lazima ifike wakati Serikali itoe majibu ya uhakika kuhusu hali halisi ya Mto wa Mbu " amesema Lowassa.
Hata Hivyo, amesema lazima changamoto hiyo ijibiwe na serikali kwa kupitia andiko la kudumu litakalo husu eneo lote la Mto wa Mbu pamoja na namna ya kupunguza tope kwenye ziwa manyara lilipo Mto wa Mbu ili kuliokoa eneo hilo.
Aidha katika kuhitimisha ombi hilo ameendelea kuwahidi wananchi wa Mto wa Mbu kuwa ataendelea kuiomba Serikali kwa msisitizo zaidi kwa kupitia Bunge kutatua changamoto hiyo pamoja na changamoto zingine za miundombinu tajika katika kata hiyo.
Na Obed Emmanuel
TEHAMA
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli