Nimegundua Wananchi wa Kijiji cha Loorela wakulima na wafugaji hawana shida katika kuchangia miradi ya maendeleo katika eneo lao hasa katika hili la u jenzi wa nyumba ya walimu. kwani maneno haya yanathibitika kupitia hiki kinachoonekana hapa leo. Baada ya kuomba kujengewa nyumba ya walimu tiyali wamechukua hatua ya kuleta kokoto, mchanga bila hata kusubiria.
Hayo yamesemwa leo Octoba 29, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Festo Shem Kiswaga wakati akizidua ujenzi wa nyumba ya walimu (two in one) wenye thamani ya Tsh.92.4 katika Shule ya Msingi Loorela Kijiji kinacho nufaika na mpango wa kaya maskini inayotarajiwa kuwa na vyumba vitatu (3) vya kulala.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo Bi.Crensia Pius Shine ambaye ni Mratibu wa TASAF Wilaya ya Monduli amesema " Shule ya Loorela yenye jumla ya wanafunzi 269 na walimu watatu (3) imepata mradi huo wa thamani ya milioni 92.4 unaotekezwa na TASAF awamu ya tatu na OPEC awamu ya nne kutokana na ombi la wananchi hao lililoibuliwa Oktoba 12, 2022 katika mkutano mkuu maalum wa wananchi hao, ambapo wananchi wenyewe walikubaliana kuchangia nguvu kazi pamoja na mawe, kokoto, Mchanga, Maji, pamoja na kulinda vifaa vyote vitakavyonunuliwa na kuhifadhiwa katika eneo lao."
Naye Bi.Happiness R.Laizer Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ametoa Rai kwa wananchi kutunza vifaa vya ujenzi vizuri na hata ujenzi ukikamilika vitakavyobaki virudishwe ghalani kwa matumizi mengine baadae.
Ameongeza kusema kuwa kupatikana kwa nyumba ya walimu kutaleta tija katika Shule yetu ya Loorela sambamba na kuimarisha utaratibu wa usalama wa Mali za Serikali zilizopo shuleni hapo kutokana na uwepo walimu katika maeneo ya Shule kila wakati.
Kwa upande wake Ndg.Johnson Loleku Mwalimu Mkuu wa Shule ya Loorela amefurahishwa sana kupata mradi huu kwani jambo hili litapunguza adha ya walimu kutoka mbali kuja shuleni kuendelea na shughuli zao za ufundishaji.
Akisisitiza Ujenzi huo, DC Kiswaga amempa fundi wa jengo hilo siku tisini (90) yaani miezi (3) kukamilisha ujenzi huo, huku akimtaka Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kufuatilia ujenzi huo na kuhakikisha ubora wake katika ujenzi wa Msingi umwaga jamvi na hatua nyingine za ujenzi zinazingatiwa na kwa viwango vilevile vya Serikali.
Akihitimisha DC Kiswaga amewaeleza wananchi kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameleta pesa nyingi Monduli hivyo tuhakikishe zinatumika kama zinavyokusudiwa kwa maendeleo ya wana Loorela Wilayani Monduli.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli