Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.Festo Kiswaga amehudhurua mkutano wa kutatua na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Tukusi chenye vitongoji vitatu (3) Chemchem,Makao mapya na Nkweri kilichopo wilayani Monduli mapema leo tarehe 6.6.2024.
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Tukusi DC Kiswagwa Mara baada ya kuwasikiliza wananchi pamoja na viongozi mbalimbali ngazi vijijiji ameeleza mbele ya wananchi kuwa "kwakuwa wote tuliridhia ugawaji wa mashamba uwe kwa watu (87) kwa kila kitongoji watu (27) mbele ya mkutano mkuu uliofanyika katika kijiji hiki basi nivyema wote tusikilizane nakueza kutatua mgogoro huu"
Kwa upande wa wenyekiti wa vitongoji vya Tukusi wameeleza kuwa makubaliano ya mkutano mkuu wa kijiji uliofanyika wananchi kutoka katika vitongoji vyote vitatu waliridhia kuwa kila mwananchi aliepitishwa kwenye mkutano huo na wajumbe hulipa sh.130,000 ili kupata eneo la shamba.
"Ukikosa mwenzako akipata sahihi sababu sio kila mwaka tutapata tunaenda kwa awamu na tuache swala la uchochezi usio na msingi,wameua viongozi waliopita acheni kusumbua wengine uku nikukosa madaraka,wazee tuwe na busara na sio kuchochea migogoro kwenye mikutano"amesema Lengere Lekoko mkazi wa Tukusi
Vivyohivyo pia wananchi wameelezwa mapato na matumizi ya ugawaji wa mashamba tsh.10,530,000 ambapo fedha hii wananchi 50 wametoa bado wananchi 30 mgawanyiko wa matumizi wa fedha ambazo zimekusanywa zimewekwa wazi ambapo Mhe.festo Kiswaga ametoa maelekezo kwa wanakijiji ambao bado awakutoa fedha hiyo watoe na mwisho wakutoa ni tarehe 30.6.2024.ili kuweka utaratibu na kuanza kujenga ofisi ya kijiji.
Akihitimisha mkutano huo mkuu wa wilaya ya Monduli amesema anahesabu mgogoro wa shamba umeisha nakutaka kusikia wananchi wanafanya maendeleo tu na sio kupishana.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli