Nawaasa enyi Vijana wote mnaohitimu hivi leo, kuweni na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwani vijana wengi mnapoteza muda mitandaoni bila faida yoyote, pia epukeni kudanganywa na makundi ya uharifu kwani kwa kufanya hivyo mtakuwa mmelisaliti Taifa lenu.
Hayo yamesemwa Aprili16, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo Shem Kiswaga wakati akitoa hotuba katika hafla ya kufunga mafunzo ya vijana wa kujitolea wa Jeshi la kujenga Taifa(JKT)kikosi namba 839 yaliyoanza Desemba 24, 2025 kikosini hapo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Kiswaga amewataka vijana hao kwenda kuyatumia vizuri mafunzo hayo waliyopata kikosini hapo kuimarisha amani ndani ya nchi yetu hasa tunapoelekea kipindi cha uchaguzi Mkuu unaotarajia kifanyika Oktoba, 2025.
Naye, Andrea Denis Lwanda Luteni Kanali ambaye ni Kamanda wa kikosi cha 839 Makuyuni; ameeleza kuwa lengo la mafunzo haya ni kuwafundisha vijana uzalendo pamoja na kuwajengea uwezo kwa kupata stadi za maisha zitakazowawezesha kuyakabili maisha baada ya mafunzo haya.
Kwa upande wake Kanali George Barongo Kazaula mwakilishi wa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajab Mabele,
alisisitiza kuwa mafunzo haya ni mwendelezo wa maono ya Mwasisi wa Taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye aliweka Msingi wa kuwaandaa vijana kwa matumizi ya elimu waliyopata ili kuilinda na kuitetea nchi yao.
Aidha, Brigedia Jenerali Mwilambege Justas Kitta,l Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Jacob Mkunda alieleza kuwa mafunzo waliyopata vijana hao yana uwezo wa kumfanya kijana kuwa hodari, mwenye nidhamu, mzalendo, na ambaye yuko tayari kulitumikia taifa huku akipongeza vijana kwa kukubali kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa na kuzingatia mafunzo ya kijeshi kwa juhudi kubwa.
Hafla hiyo imeambatana na matukio mbalimbali ikiwemo maenesho ya kwata, singe, kufunga na kufungua silaha ngoma na muziki
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli