Mwenyekiti wa Mkutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness R. Laizer, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, leo Agost 11, 2025 katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo ameongoza Mkutano wenye lengo la kupokea taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa katika Kata zao Wilayani humo.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika Kata ya Lolkisale Ndg. Laban Joseph ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata hiyo (WEO) ameeleza kuwa Kijiji hicho chenye jumla ya Wakazi 9466 Kinajishughulisha na kilimo, ufugaji na Biashara ndogo ndogo.
Aidha, Ndg. Laban Joseph ameomba Mkutano huo wa Halmashauri kukipatia Kijiji hicho Watumishi wawili wa kada za Wanyama pori na Misitu ili kukidhi mahitaji kulingana na upungufu uliopo.
Sambamba na hilo, Maafisa Watendaji wa Kata za Lolkisale, Lepurko, Mfereji, Meserani, Engutoto na Monduli juu wameuomba Mkutano huo wa Halmashauri kuandaa mafunzo ya pamoja kwa mabaraza ya Kata ili kuyawezesha mabaraza hayo kufanya shughuli zake kwa Weledi na ufasaha zaidi kwa Maendeleo ya Halmashauri hiyo.
Bi. Happiness R. Laizer amewataka Watendaji hao kutoa hamasa kubwa katika Kata zao kwa kuanza na viongozi ndani ya maeneo yao na baadae Wananchi ili wajenge vyoo bora na kuvitumia huku akisisitiza Watendaji kusimamia vema ujenzi na ukarabati wa vyoo katika maeneo ya minada ili kulinda Afya za Wananchi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli