Tusipotunza miundombinu hii ya maji tuliyofadhiliwa na The International Ministry of Jesus, na Mazingira yanayouzunguka changamoto ya maji haitaisha hivyo tunao wajibu wa kuutunza ili mradi huo utufae kwa sasa na baadae.
Hayo yamesemwa leo Septemba 15, 2025 na Mhe. Gloriana Julius Kimath wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Lemooti katika hafla fupi ya Uzinduzi wa Mradi wa maji uliogharimu jumla ya shilingi milioni 126 kutoka kwa wafadhili hao
Akisoma taarifa ya mradi huo wa maji katika Kijiji cha Lemooti Kata ya Lemooti Ndg. Lucas Munis mmoja wa wasimamizi wa Mradi huo amesema kuwa, mradi huo umegharimu jumla ya Shilingi milioni 126 ambapo shilingi milioni 124 zimetolewa na wafadhili wa The International Ministry of Jesus na shilingi milioni 2 zikichangiwa na Wananchi wa Kijiji hicho na mradi huo utahudumia jumla ya Wakazi 2000 wa Kijiji hicho.
Ndg. Lucas Munis ameeleza kuwa mradi huo wa kisima umekamilika kwa sasa na unaweza kutoa takriban Lita 4,000 na umefungiwa pump yenye horse power 5.5 kwa ajili ya kusukuma maji.
Aidha, Ndg. Lucas ameeleza changamoto kubwa inayoukabili mradi huo ni ukosefu wa Umeme kwaajili ya kusambaza miundombinu ya maji hayo kwenye Taasisi na maeneo ya makazi ya watu.

Naye Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo amelishukuru shirika la International Ministry of Jesus kutoka Marekani kwa kufadhili mradi huo ambao unagusa wananchi wa kizazi hiki na vizazi vijavyo; huku akiwataka wananchi kuutunza na kupanda miti kwenye chanzo na maeneo yanayozunguka mradi huo.
Kwa upande wake Bi. Janeth Madee amewashukuru wafadhili kwa kuiona Lemooti kuwa ni moja kati ya vijiji vyenye uhitaji wa maji nakutufadhili kwani awali tulikuwa na shida kubwa kwetu na Mifugo.
Mhe. Gloriana amewataka wafadhili hao kuendelea kusaidia vijiji vingine Wilayani Monduli kupata maji kwa ndio changamoto kubwaWilayani humo huku akiwasisitiza Wananchi wa Lemooti kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025

Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli