Jukumu letu kama Watumishi ni kutoa huduma kwa wananchi, ukizingatia kwamba Jamii ya Wananchi wa Monduli ni wafugaji hivyo kupata Vitendea kazi hivi vitasaidia sana kuwahudumia wananchi kwa karibu na kwa wakati.
Hayo yamesemwa leo Septemba 15, 2025 na Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli katika zoezi rasmi la kukabidhi jumla ya Vitendea kazi 526 ikiwemo vishikwambi 46, Cool box 25, Gunboot pair 15, Overall Pcs 15, Automatic syringe 25, na Needle 400.
Naye Dkt. Yandu Marmo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatia vifaa kwa ajili ya utambuzi wa chanjo za Mifugo, ambapo jumla ya ng'ombe laki mbili na themanini (280,000), mbuzi na kondoo laki sita (600,000) zinatarajiwa kuchanjwa, pamoja na kuku zaidi ya laki tatu 300,000) ambao watachanjwa chanjo ya tatu moja.
Bi. Happiness R. Laizer amehitimisha zoezi hilo kwa kuwaeleza Watumishi hao kuwa wanalo deni la kutoa huduma bora kwa wananchi ili waendelee kuipenda Serikali yao ya awamu ya sita.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli