Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha, Mhe.Kenan Laban Kihongosi @kenanikihongosi amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Ndugu Paul Makonda na kuanza kazi rasmi na kuhudhuriwa na viongozi wa Chama na Serikali, watumishi wa Umma, viongozi wa dini, pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo rasmi mapema leo mapema leo Juni 30, 2025.
Hafla hiyo ilianza kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda, kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu na shughuli za utekelezaji wa mkoa huo huku akieleza mafanikio yaliyopatikana kisekta kwa kipindi chote alichohudumu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu mpya wa Mkoa Mhe. Kihongosi, amemshukuru Mwenyenzi Mungu kupitia Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan kwa imani yake kubwa na kumpa dhamana ya kuongoza Mkoa wa Arusha na kumshukuru Mtangulizi wake Ndugu Makonda kwa kazi kubwa aliyoifanya katika mkoa huo, kazi ambayo ameacha alama kubwa mkoani hapo.
"Mhe.Rais amenituma Arusha kuja kuwatumikia wananchi wa Arusha na nimekuja kufanya kazi, ninachoomba kwenu ni ushirikiano ili kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo, tukiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wa Arusha wanafurahia matunda ya nchi yao". Ameweka wazi Mhe.Kihongosi
Aidha, amesisitiza kutoruhusu kikwazo chochote kitakachojaribu kuzuia agenda ya maendeleo katika utendajinkazi, wajibu wake ni kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiweo matumizi sahihi ya fedha za Umma zinazoletwa kwa ajaili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta zote.
Zaidi amewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kwa kusimamia Kanuni, Sheria na taratibu kwa kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wote, ili i kila mtua aweze kufurahia matunda ya Serikali na Nchi yake.
Sambamba na hayo, Mhe.Kihongosi amehamishiwa Mkoani Arusha akitokea Mkoa wa Simiyu ambapo, ameagizwa na Mhe. Rais kuwaaunganisha wananchi wa Mkoa huo.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli