Ninawapongeza sana kwa hatua hii kubwa mliyoifikia ya kupunguza vifo vya akina Mama na watoto wachanga vinavyotokana na uzazi kutoka vifo vitatu(3) hadi kimoja(1) pamoja na kuongeza idadi ya Wanawake wanaojifungulia katika hospitali zetu kutoka 4,476 hadi 5,900 kwa mwaka 2023/2024.
Hayo yamesemwa leo Juni 14, 2025 na Bi. Pamela Ijumba kwa niaba ya Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, alipokuwa akizungumza na Wauguzi wa vituo vya afya na wa hospitali ya Wilaya hiyo katika maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani ambayo Ki Wilaya yamefanyika katika viwanja vya kituo cha afya Mto wa Mbu Wilayani humo.
Bi. Pamela amewaeleza Wauguzi hao kuwa, " Ninyi ni injini katika Idara ya Afya kutokana na umuhimu wenu kwa kusaidia kuokoa maisha ya watu Duniani hivyo tunatarajia kuwa mntaendelea kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kuzingatia Sheria, miongozo, na taratibu kama alivyofanya mwasisi wenu Bi. Florence Nightingale." amesema Bi. Pamela
Akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wauguzi hao
Bi. Epifania Mratibu wa afya ya Uzazi Wilaya, ametaja mafanikio makubwa yaliyofikiwa kwa mwaka 2025 kuwa ni pamoja :- kufanya kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na Uzazi kutoka vifo vitatu hadi kimoja kwa mwaka 202/2024, kuongeza idadi ya wamama wanaojifungulia hospitali kutoka 4,476 hadi 5,900 kwa mwaka 2023/2024, kukusanya damu salama, kufanya uchunguzi wa saratani ya mlango wa Uzazi na matiti, uchunguzi wa homa ya ini na kutoa chanjo yake, kutoa huduma ya dawa za ganzi na usingizi, kupima shinikizo la damu, kutoa elimu ya Malezi na Makuzi pamoja na kuhudumia wagonjwa wa ndani na wa nje.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt. George Kasibante amewataka Wauguzi hao kutoa huduma bora kwa wagonjwa, kujitoa, na kwa wale ambao bado hawawajibiki vizuri wabadilike haraka sana kwakuwa Mazingira ya kazi yameboreshwa, dawa zipo, na miundombinu imeboreka katika kila vituo vya afya
Naye Bi. Rose Yongolo Mwenyekiti wa Wauguzi hao amewashauri Wauguzi wenzake kufanya kazi kwa kufuata maadili na mienendo ya mwasisi wao Bi. Florence Nightingale huku akieleza kuwa mishumaa waliyoiwasha wakati wa kula kiapo cha uadilifu iwakunbushe namna ambavyo Bi. Florence alitumia Nuru hiyo kwenda kila mahali kutoa huduma kwenye vita ya pili ya Dunia - Cremean war vivyo hivyo na wao watoe huduma kwa wagonjwa.
Bi. Pamela Ijumba amehitimisha kwa kuwataka Wauguzi hao walio tayari kujifunza suala la utoaji wa ganzi tiba na usingizi kufanya hivyo kwani Bajeti ipo.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli