Mwenyekiti wa Mkutano wa Halmashauri, Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, leo Agost 11, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri amewaongoza wajumbe wa Mkutano huo kupokea na kujadili kwa kina taarifa za Kamati za Kudumu za halmashauri robo ya nne April Hadi Juni 2024/2025.
Katika Mkutano huo Taarifa za Kamati mbalimbali zikiwemo Kamati shirikishi ya UKIMWI, Elimu, Afya na Maji, Uchumi, Ujenzi na Mazingira pamoja na Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango zimepokelewa na kujadiliwa kwa kina.
Akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Fedha, Utawala, na Mipango, Bi. Gwantwa Sema ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu ameeleza changamoto mbalimbali zilizobainishwa na Kamati hiyo ikiwemo changamoto ya upungufu na ukosefu wa Maji Wilayani humo hasa wakati wa kiangazi huku akiuomba Mkutano huo kuweka mpango wa namna bora ya kushuguulikia changamoto hiyo.
Aidha, Bi. Gwantwa Seme ameeleza suala la Ulinzi wa ardhi ya watu asilia kuwa ni muhimu ili ardhi yao isiuzwe wala kuvamiwa kwa ajili ya urithi wa vizazi vijavyo.
Bi. Happiness R. Laizer, Mwenyekiti wa Mkutano huo amewasisitiza wajumbe kufanya kazi kwa Weledi hasa katika kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli