Nitafanya ufuatiliaji wa mara kwa mara hasa katika suala la utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na ukusanyaji wa mapato ndani ya Wilaya yetu, kwa Lengo la kusaidia Halmashauri kuhakikisha inakamilisha miradi ya maendeleo kwa wakati pia kufikia lengo la ukusanyaji mapato tuliyojiwekea.
Hayo yamesemwa leo Agost 13, 2025 na Mhe. Gloriana J. Kimath Mkuu wa Wilaya ya Monduli katika kikao kazi na Wakuu wa Divisheni na Vitengo kilichofanyika katika Ukumbi mdogo wa mikutano wa Halmashauri hiyo, chenye lengo la kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo Wilayani humo.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi yenye jumla ya Shilingi Bilioni 2.4inayotekelezwa Wilayani humo kupitia Serikali kuu, Mapato ya ndani, BOOST, WASH,TASAF, LANES na Mfuko wa Jimbo;Ndg. Abraham Msofe kwa niaba ya Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Ndg. Lucas H. Daud amesema
"Miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo inaendelea kukamilishwa ikiwemo ujenzi wa zahanati, mabweni, madarasa na vyoo haikukamilika kwa wakati kwa sababu ya kuchelewa kwa fedha za ukamilishaji wake na nyingine kufika mwishoni mwa mwaka huo wa fedha na changamoto ya wazabuni. Ambapo kwa sasa inaendelea kukamilishwa na itakamilika kwa wakati. " amewasilisha Ndg. Msofe
Naye Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo ameeleza kuwa,kwa suala la wazabuni baada ya kubaini changamoto tulikaa nao nakuwahamasisha kuomba zabuni kupitia mfumo wa NEST pamoja na kuwaeleza mikakati iliyowekwa kuhakikisha wanaodai wanalipwa kwa Bajeti iliyotengwa ili kuweka uaminifu kwa wazabuni hao kuendelea na kazi.
Mhe. Gloriana ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kutoa Elimu kwa mara nyingine kwa Wazabuni hao ili wawe na Elimu ya kutosha ya namna ya kuomba zabuni kwenye mfumo wa manunuzi wa NEST ili wawe na uelewa zaidi ili kupunguza changamoto ya uchelewashaji na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo Wilayani humo.
Sambamba na hayo Bi. Gloriana ameelekeza miradi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kutekeleza kwa Weledi na kwa kuzingatia ubora unaokubakika na ikamilike kwa wakati.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli