Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, jumla ya Hospitali za wilaya 129 zimejengwa kote nchini ikiwa ni jitihada za kuboresha huduma za afya Kwa watanzania mijini na vijijini.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo Sept. 19, 2024 wakati kizindua Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) katika hospitali ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Vilevile amesema kuwa Rais Samia amefanikiwa kukarabati hospitali kongwe zaidi ya 28, Monduli ikiwa miongoni mwa Wilaya zilizo nufaika na ukarabati huo.
"Jengo hili ambalo mmenipa heshima ya kuja kulizindua nataka niwathibitishie kuwa kiwango hiki cha fedha kilichoingia Monduli kimekwenda nchi nzima katika hospitali kongwe zilizojengwa miaka ya 1960 na 1970.'' Hivyo jengo hili lililozinduliwa leo lina thamani ya zaidi ya milioni 460 na Lina uwezo wa kuhudumia wagonjwa takribani laki mbili.
Akiwa ameambatana na Mhe. Paulo Makonda Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe Mchengerwa ametumia nafasi hiyo kukemea uzembe kwa wataalamu wa afya, na kusema kuwa suala la uzembe limekuwa likisababisha vifo vingi vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Mhe. Waziri Mchengerwa amehitimisha kwa kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Monduli kwa kuwa mstari wa mbele kutekeleza agizo lililotolewa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi yake juu ya suala la kuhimiza huduma bora kwa Wateja ambapo Monduli tiyari mmetekeleza kwa kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wa Idara ya Afya.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli