Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe. Fredrick Lowassa amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa takribani Bilioni 37 kwaajili ya kutekeleza miradi ya Maji wilayani Monduli na hivyo kuwaondoa wananchi wengi kwenye adha ya kusafiri umbali mrefu na kutumia muda mrefu kutafuta huduma ya maji.
Akizindua mradi wa maji Kitongoji cha Imorijo leo Machi 18, 2025, hafla iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Wiki ya maji mkoa wa Arusha, Mhe. Lowassa amekiri kuwa kuna maeneo wananchi wake walikuwa hawajawahi kuona huduma ya maji ya bomba ikiwemo Nanja na Sepeko lakini kupitia mapenzi makubwa ya Rais Samia kwa wananchi wake, Vijiji hivyo kwasasa vinafaidika na utawala wa Rais Samia kupitia maji safi, salama na ya uhakika.
Maji ni jambo la kihistoria Monduli yetu, wakati wa uongozi wa Mzee (Hayati Edward Lowassa) teknolojia haikuruhusu kuchimba maji na hata nilipoingia madarakani mwaka 2020 bado changamoto ya maji ilikuwa kubwa na sikuwa na matumaini makubwa kwani niliambiwa vyanzo vya maji bado ni vya kutokea mbali na ni gharama kuvuta maji hapa, lakini kwa Mapenzi makubwa kwa wana Monduli kutoka kwa Rais Samia, leo tumefanikiwa.” Amesema Mhe. Lowassa.
Aidha kwa upande mwingine wananchi wa Monduli ambao wameendelea kunufaika na miradi hiyo ya maji inayotekelezwa Wilayani humo wameishukuru serikali kwa huduma hiyo, wakisema kwasasa wanapata muda mwingi zaidi wa kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda mrefu kusaka huduma ya maji kutokana na umbali uliokuwepo.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli