Vijana zaidi ya mia moja kumi na tatu walio maliza mafunzo ya Jeshi la akiba Wilayani Monduli wametakiwa kuishi kwa kuzingatia viapo vyao na kuleta mabadiliko chanya katika jamii wanayo izunguka.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Monduli Mhe.Festo Kiswaga wakati akifunga mafunzo ya Kozi ya Awali ya Jeshi la Akiba Wilaya ya Monduli Kundi la 42 mwaka 2024/25
Amesema kuwa vijana hao sasa wamebadilika tofauti na walivyo kuwa raia hivyo ni wajibu wao kulitumikia Taifa kama yanavyo fanya majeshi mengine kote nchini kulingana na wajibu wao lakini pia amewaasa vijana kulinda amani katika maeneo wanayoishi.
Aidha amewapongeza vijana hao kwa kuhitimu mafunzo hayo ya jeshi la akiba na kuwataka Kuwa wakakamavu na hodari katika jamii.
Vilevile Mkuu wa Wilaya ya Monduli amempongeza Mkurugenzi mtendaji Bi.Happiness Laizer Kwa kugharamia sare za Askari waliohitimu Mafunzo hayo ya Jeshi la akiba jambo ambalo limeleta umoja na kuwafanya waone Wilaya ya Monduli ipo pamoja nao.
Kwa Upande wake Mshauri wa Jeshi la akiba Meja, SA.Komba Wilayani Monduli akisoma taarifa ya mafunzo hayo amesema Jumla ya Wanafunzi waliojiandikisha ni 158, na waliomaliza ni 113 (wanaume 106, wanawake 7) huku akisisitiza askari waliomaliza kwenda Kuwa walinzi katika maeneo yao wanayoishi na kusaidia zaidi majanga yanapotokea.
Kozi hiyo ya Awali yaJeshi la Akiba Wilaya ya Monduli Kundi la 42 mwaka 2024/25 imedumu kwa wiki 19 mpaka kumaliza.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli