Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe.Festo Shem Kiswaga amekabidhi hundi ya shilingi milioni 187 kutoka Randlen (WMA) fedha za jumuiya za hifadhi kwa vijiji nane (8) katika Kata tatu za Mswakini,Lemooti,Lolkisale zilizopo Wilayani Monduli tarehe 13, Machi 2025.
Akizungumza katika hafla hiyo Mhe.Festo Kiswaga ametoa shukrani za dhati Kwa (WMA) na timu nzima kwa kuwawezesha Wananchi walioko Wilaya Monduli kunufaika na fedha hizo kwani zitawasadia kujenga madarasa kwa ajili ya wanafunzi, na kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalum ikiwa ni pamoja na kumalizia miradi ambayo haijakamilika.
Naye Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Fredrick Lowassa amemshukuru Mkuu wa Wilaya na kusema '' Jambo alilolipigania linafanyika na hata Wananchi kuweza kupata fedha za Randilen ambazo zitasadia maisha ya Mwananchi mmoja mmoja Monduli; kupitia kwako Mkuu wa Wilaya na mbele ya wananchi kwamba Serikali iweze Kuona faida za fedha za Randilen (WMA) Monduli". amesema Fredrick
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Pamela Ijumba amesema, fedha ambazo Wananchi wamepata kwaajili ya kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kufanya maendeleo mengine zifuatwe kanuni na taratibu za manunuzi ili kuhakikisha miradi inayojengwa inakuwa na ubora.
Naye Diwani wa Kata ya Lolkisale Mhe.Solomoni Kisioki ameishukuri Randlen (WMA) Kwa kuiona Kata ya Lolkisale ni miongoni mwa wanufaika wa fedha hizo, hivyo kupitia milioni 23 zilizotolewa zitaenda kujenga shule ya Msingi Kijiji Cha NAFCO ambayo itarahisisha kupunguza umbali mrefu kwa wanafunzi kwenda kujisomea shule zilizoko mbali.
Mhe.Nanga Lenasira, Diwani Kata ya Mswakini ameshukuru kwa kupata fedha hizo ambapo zitaenda kumalizia miradi ambayo haijakamilika ikiwemo nyumba za walimu pamoja na mabweni ya wanafunzi.
Mwenyekiti wa Randilen Lazaro Peter Laizer amehitimisha kwa kuwataka Wananchi wa Wilaya ya Monduli kwa vijiji nane (8) vilivyopata fedha hizo kuzitumia kwaajili ya kuleta maendeleo kwa kujenga miradi itakayo wasaidia watoto wenye mahitaji na kumalizia miradi ambayo bado haijakamilika na si Kwa matumizi mengine.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli