Mkoa wa Arusha utakuwa mwenyeji wa sherehe kubwa za kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, zitakazofanyika Machi 8, 2025, ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Maadhimisho haya yatalenga kuhamasisha usawa wa kijinsia na kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika nyanja mbalimbali za jamii.
Kwa mara ya kwanza, maadhimisho haya yatakuwa ya kipekee, ambapo sherehe zitaanza tangu Machi 1, 2025, na kudumu kwa siku saba, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Mwanamke. Katika kipindi hicho, wizara nane zitatoa huduma muhimu kwa jamii, ikiwa ni pamoja na huduma za afya, kisheria, na elimu ya fedha.
Vilevile, maadhimisho haya yatakuwa na michezo ya aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mechi za mpira wa miguu kati ya timu maarufu za wanawake, Simba Queens, Yanga princess, JKT Queens na Fountain Gate FC, ili kusherehekea ushiriki wa wanawake katika michezo.
Hii ni fursa muhimu ya kuonyesha juhudi za wanawake katika maendeleo na kujenga jamii yenye usawa wa kijinsia.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli