Nikisikia umeshalipwa pesa na kazi haiendelei nitakushughulikia. Lakini kwakuwa umeweza kufanya vizuri kwenye mradi wa Maji ndani ya Wilaya yetu basi naamini hata katika mradi huu, utafanya vizuri.
Hayo yamesemwa Feb 19, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mhe. Festo Shem Kiswaga wakati wa hafla fupi ya utiaji Saini wa Mkataba wa Mradi wa Ukarabati wa miundombinu ya Umwagiliaji katika skimu za Mto wa Mbu Wilayani Monduli.
Akisoma Taarifa ya Mradi huo Ndg. Alfred amesema kuwa mradi huo wenye thamani ya bilioni 17.6 unasainiwa kati ya Tume hiyo na M/S Jandu Plambering Limited na utadumu kwa miezi 18 ambapo, skimu zitakazo fanyiwa kazi ni kumi (10) kati ya 17 ambazo ni Mahande, Majengo juu, Kabambe Majengo, Blockfarm, Migungani, Jangwani, Kirurumo, Migombani chini na Nawaleni.
Aidha, Ndg. Aretas Nyengela Kaimu Mwandishi wa Umwagiliaji Mkoa wa Arusha amesema kuwa kazi za Mkataba huo ni kusafisha mifereji kwenye skimu, kuchimba na kujengewa mitaro ili kuzuia mafuriko, kuweka uzio(electrical fiance) kuzuia uharibifu wa mazao, wanyama pori na Mifugo.
Naye Mkurugenzi wa Tume ya Umwagiliaji Bw. Raymond William Mndolwa amemtaka mkandalasi kuhakikisha anaboresha barabara za kueleleka kwenye skimu hizo ili kurahisisha usafirishaji wa mazao huku akisisitiza kuwa kujenga uzio huo isiwe chanzo cha vyuma chakavu bali iwe ni kulinda mazao ya wakulima katika skimu hizo.
Kwa upande wake Mhe. Fred Lowassa - Mbunge wa Monduli amemtaka Mkandalasi aliyesaini Mkataba huo kutoa fursa kubwa za ajira kwa wananchi wa maeneo ya mradi ili waweze kunufaika na mradi huo tangu hatua za ujenzi wake.
Bi. Happiness R. Laizer Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ametoa shukrani kwa Tume ya umwagiliziaji na kusema kuwa anaamini uzalishaji wa mazao utaongezeka huku akiwataka wananchi kuchukuwa tahadhali mara itakapowekwa fensi ya umeme ili yasitokee madhara kwa binadamu sambamba na kumwelekeza Afisa kilimo kuandaa mbegu Bora ili wananchi waanze kuzalisha kwa tija.
Kwa niaba ya wananchi wanufaika wa mradi huo Bi. Hellena Mollel ametoa shukrani kwa uongozi wa awamu ya sita kwa kuwakumbuka wakulima wa Monduli na kuomba viongozi husika kusaidia kuboresha bei za mazao yao.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli