Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Dkt.George Kasibante akiambatana na Mganga Mfawidhi Dkt. Godfrey Kahamba na Roman Living Minja ambaye ni Afisa afya na pia Mwakilishi wa Primary Health Care Council Initiative and innovation Wilayani humo; wameshiriki Mkutano wa 12 wa Mwaka 2025 Tanzania Health Summit (THS) unaofanyika Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 1 hadi 3, 2025 katika ukumbi wa Kimataifa wa Nyerere (JNICC ).

Ambapo mkutano huo una lengo la kujadili juu ya matumizi sahihi ya Takwimu na teknolojia ili kuongeza kasi ya upatikaniaji wa huduma za afya kwa watu wote Nchini kwa mstakabali wa afya njema ya Taifa na Wananchi kwa ujumla.

Mkutano huo ulioandaliwa na Tanzania Health Summit (THS) kwa kushirikiana na Wizara Afya na Wadau mbalimbali katika sekta hiyo, umekutanisha washiriki kutoka Wizara ya Afya, wakiwemo Makatibu, watu Mashuhuri, Mabalozi, Mashirika ya Maendeleo ya Afya Duniani (WHO), Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UNCEF) , UNFPA, Benki kuu ya Dunia, Viongozi kutoka Asasi zisizo za kiserikali ndani na nje ya Nchi pamoja na washiriki zaidi ya elfu mbili na miatano.

Katika Mkutano huo mkubwa wa Kitaifa na Kimataifa, Ndg. Roman Living Minja Afisa Afya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ameiwakilisha vyema Halmashauri hiyo Kwa kuibuka Mshindi wa kwanza katika category ya Ntuli A. Kapologwe Primary Health Care Implementor Award na kutwaa Tuzo pamoja na Medali katika kutambua Umahiri, Kujitolea, Ubunifu na Uongozi katika kuimarisha Mfumo wa huduma za Afya ya Msingi kwa ajili ya Ustawi bora wa Jamii.

Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli