
Ninaamini, mafunzo haya ya siku tatu mliyoyapata yatawawezesha kutimiza majukumu na wajibu wenu kwa Weledi, usahihi na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na maadili ya Utumishi wa umma.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 15, 2025 na Bi. Pamela Ijumba Mkuu wa Divisheni ya Kilimo na Mifugo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Happiness Raphael Laizer; alipokuwa akifunga rasmi mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo Maafisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Monduli yaliyofanyika katika Ukumbi wa Naramatisho Women Centre uliopo Kata ya Makuyuni Wilayani Monduli.

Naye Dkt. George Kasibante ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli amewaeleza Maafisa Ustawi wa Jamii hao, umuhimu wa kutoa taarifa sahihi, kwa wakati na kwa kuzingatia makundi sita muhimu ndani ya Jamii wakiwemo Wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.
Bi. Pamela ametoa shukrani kwa Shirika la Pastorate Women Council (PWC) kupitia Bi. Nalemuta Moisan ambaye ni Mratibu wa haki na uongozi wa wanawake wa Shirika la hilo kwa kuendelea kuisaidia Jamii ya Wana Monduli.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli