Katibu wa NEC-Itikadi, uenezi na Mafunzo CCM Taifa Ndg. CPA Amos Makalla amefanya mazungumzo na Wananchi wa Wilaya ya Monduli Kwenye uwanja wa Mkunguni mto wa mbu Leo septemba 07, 2024 ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake Katika Mikoa yote ya Tanzania akiwa na malengo manne muhimu.
Akizungumza na Wananchi Wilayani Monduli Ndg. CPA Makalla amesema " Katika ziara hii nimepita mikoa 17 ya Tanzania na malengo makuu ni manne tu ambayo ni:-
1. Kuangalia uhai wa chama Cha mapinduzi
2. Kueleza maandalizi ya uchaguzi ujao
3. Kuongelea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi
4. Kusikiliza kero za Wananchi na kuzitatua.''
Akifafanua zaidi malengo hayo Ndg. CPA Makalla ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi ni Imara na ndicho chama pekee chenye dhamana na matumaini Kwa Wananchi, Chama kinacho ahidi na kutekeleza sambamba na kutatua matatizo na kuwaletea Wananchi maendeleo, hivyo amewaomba Wananchi kujitokeza Kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wakazi Kwa Kila Kijiji kuanzia tarehe 11 Oktoba hadi 20 Oktoba, 2024 kwani kufanya hivyo Kwa wingi kutatupatia uhakika wa kura zetu kutosha.
Ameongeza kuwa Dr. Samia Suluhu Hassan ni Rais pekee ambaye ameleta na anazidi kuleta fedha nyingi Kwa ajili ya maendeleo hivyo Kwa vijiji vyote 62 na vitongoji vyake kura zote ziwe za CCM.
Ndg. CPA Makalla amesisitiza kuwa Wananchi waendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi Kwa kuwa ni Imara na kitahakikisha Katika chaguzi zijazo viongozi wote wasio na sifa na ambao hawakuweza kutatua changamoto za Wananchi Wala kusoma taarifa za mapato na matumizi na ni wa CCM, hatutawahitaji badala yake tutawaletea wagombea safi kutoka CCM watakaoendana na sera na kasi ya Rais wetu.
Akihitimisha mazungumzo hayo Katika uwanja wa Makunguni mto wa mbu, CPA Makalla ametoa wito na kuwatahadharisha Wana Monduli kuwa Tanzania ni moja hivyo Wananchi muwe macho na wanasiasa wanaochukuwa changamoto za Wananchi Kwa faida zao binafisi.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli