Timu ya Menejimenti (CMT) ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ikiongozwa na Bi. Happiness Raphael Laizer - Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, leo Oktoba 6, 2025 imetembelea na kukagua jumla ya miradi ya maendeleo 17; yenye thamani ya jumla ya Tsh. Bilioni 1.3 inayotekelezwa Wilayani humo kwa fedha kutoka Serikali kuu, Wahisani ( BOOST, SWASH, EP4R na LANES ), nguvu za wananchi na mapato ya ndanI.

Aidha, Timu hiyo ya CMT kwa makundi, imeweza kutembelea na kukagua miradi yote hiyo inatekelezwa katika Kata za Sepeko, Makuyuni, Mswakini, Esilalei, Lolkisale, Moita, Monduli juu, Naalarami na Engutoto; ambapo miradi IPO katika hatua mbalimbali kama vile hatua ya Msingi, hatua ya kupandisha, hatua ya kufunga lenta na hatua ya umaliziaji.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Lowasa Mwl. Sayuni A. Tarimo Mkuu wa Shule ya Sekondari Lowasa amesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Lowasa unajumuisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya awali na matundu sita ya vyoo sambamba na shule ya Msingi ya mkondo mmoja yenye vyumba sita vya madarasa na vyoo matundu kumi, jengo la Utawala na kichomea taka ambapo ujenzi umeanza rasmi Septemba 4, 2025 na unatarajiwa kukamilika Desemba 31, 2025.

Kwa upande wake Ndg. Jofrey Nditolo Mwambasi, Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu ameshukuru kwa ushirikiano kutoka kwa Watumiaji kwa kila mradi katika kuhakikisha miradi inasimamiwa kwa usahihi na kwamba itakamilika kwa wakati.

Kufuatia ukaguzi huo wa miradi, Bi. Happiness Raphael Laizer amewataka wasimamizi wa miradi kwa kila mradi, kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaokubarika.

Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli