USHURU WA HOTELI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI
Kodi hii ni matokeo ya Sheria ya fedha namba 9 ya 1982 kifungu cha 6 (1)(U).
Kodi hii hulipwa na makampuni, taasisi na biashara mbalimbali zilizosajiliwa VAT. Kutokana na mauzo ghafi kwa kiwango kisichozidi asilimia 0.3.
Aina ya Makosa yatakayosababisha kutozwa faini/adhabu:-
· Mtu yoyote anayetakiwa kulipa kodi akishindwa kuwasilisha hesabu zake kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ndogo na inapobainika kuwa amefanya makundi.
.
· Mtu yoyote ambaye bila sababu za msingi atashindwa:-
(a) kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa kwa Halmashauri katika muda uliowekwa.
(b) Kutunza kumbukumbu, kitabu au hesabu.
(c) Kuonyesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi.
Mtu yeyote bila sababu za msingi:-
(a) Akifanya hesabu za uongo kwa kupunguza au kutoa hesabu zisizokuwa sahihi.
(b) Akitoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu jambo lolote linaloweza kuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa kodi.
(c) Akiandaa au kutengenezewa vitabu vya uongo vya Mahesabu au kumbukumbu.
(d) Atamzuia au atajaribu kumzuia Afisa Muidhiniwa kutekeleza majukumu yake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ndogo atakuwa anatenda kosa.
NB: Pamoja na adhabu atakayotozwa mkosaji kwenye kif. Na. 17 (1). Pia atawajibika kulipa gharama nyingine za Halmashauri.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli