Leseni, Vibali, Kodi, Fomu za sajil
SHERIA NA TARATIBU ZA KUPATA HUDUMA ZA LESENI HALMASHAURI YA WILAYA YA MONDULI
Na. |
SHERIA / KANUNI |
UTARATIBU WA KUFUATWA |
MUHUSIKA |
MWASILIANO
|
1
|
Sheria ya leseni za biashara Na 25 ya 1972
|
Kujaza fomu ya maombi (Fomu Na tfn21) na kuambatanisha nyaraka zifuatazo
- Kwa jina la biashara aweke nakala ya hati ya kuandikisha jina la biashara au kampuni kutoka BRELA - Hati ya uthibitisho wa uraia (Anaweza kuweka cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo cha Mahakama) - Uthibitisho wa kuwa na mahali [pa kufanyia biashara( Hati ya nyumba au mkataba wa pango au stakabadhi ya malipo ya kodi ya majengo) - Hati ya kusajiliwa kama Mlipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Pamoja na hati ya utakaso ya kulipa kodi(Tax clearance Certificate) - Kwa waombaji ambao sio raia wa Tanzania wawe na hati ya kuishi nchini ya daraja ‘A’ na kwa wawakilishi wa mfanyabishara au kampuni iliyoko nje ya nchi wawe na hati ya Kiwakili ( Power of Attorney) - Kwa biashara za kitaalamu awe na cheti cha utalaamu - Kwa biashara zinazodhibitiwa na Mamlaka za udhibiti awe na hati kutoka Mamlaka husika. Kwa waombaji wanao huisha leseni zao watajaza fomu ya maombi na kuambatisha nakala ya leseni ya kipindi kilichopita. |
Abdallah A. Magambo Afisa Biashra wa Wilaya Monduli Shamimu Shabani Afisa Biashara William Ushaki Afisa Biashara |
0756- 488578
0759-869510 0659390052 |
2
|
Sheria ya leseni za vileo Na 28 ya 1968 na marekebishao yake ya 2012 |
Muombaji atajaza fomu ya maombi
- Atatakiwa kuambataisha Hati ya Mlipa kodi-TIN kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Pamoja na hati ya utakaso ya kulipa kodi(Tax clearance Certificate) - Kwa waombaji wapya fomu ipitishwe kwa; a) Kwa Afisa Afya wa kata b) Afisa Mtendaji wa Kijiji/Kata c) Afisa Biashara - Kwa waombaji wanaohuisha leseni watajaza fomu ya maombi na kuambatisha nakala ya leseni ya kipindi kilichopita na kupitisha fomu |
Shamimu Shabani Afisa Biashara William Ushaki Afisa Biashara |
0759-869510
0659390052 |
3
|
Hotel levy Act ya 1973 |
Kodi hii hulipwa mara moja kabla ya tarehe 7 ya kila mwaezi. Mlipaji anatakiwa kuja na kitabu cha wageni, Afisa Biashara husika hukokotoa kiasi cha kodi kutoka katika kitabu cha wageni. Kiasi cha kodi ni asilimia kumi ya mapato ya mwezi
|
Shamimu Shabani Afisa Biashara William Ushaki Afisa Biashara |
0759-869510
0659390052 |
4
|
Mabango: sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa sura ya 288 kifungu Na. 89 (1) |
kujaza fomu ya maombi na kuiwasilisha kwenye ofisi ya mapato kisha Afisa husika kwenda eneo husika kwa ukaguzi ili kubaini ukubwa na aina ya bango aidha kujiridhisha kama eneo linafaa kwa shughuli hiyo.
|
Gaudance Seleka Mhasibu Mapato Abdallah A. Magambo Afisa Biashara Eng. Daudi Sebyiga Mhandisi(w) |
0752-931747
0756-488578 0754-447725 |
5
|
Nyuma na Vibanda vya Halmashauri |
Kufika ofisi ya Mapato ya Halmashauri na kupewa Hati ya Malipo(Bill) kwa ajili ya malipo
|
Shamimu Shabani Afisa Biashara Gaudance Seleka Mhasibu Mapato |
0759-869510
0752-931747 |
6
|
Kodi ya huduma ya (Service levy) sheria ya Fedha ya Serikali za mitaa sura ya 290 kifungu Na. 6 (01) na 16 (1) |
Kujaza fomu na kuiwasilisha kwa Afisa husika kwaajili ya ukokotoaji wa kiasi cha kodi inayopaswa kulipwa. Tozo ni asilimia 0.3(0.3% ya mapato ya kipindi husika baada ya kutoa VAT na kodi zote alizolipa Serikalini
|
Gaudance Seleka Mhasibu Mapato Abdallah A. Magambo Afisa Biashara(W) |
0752-931747 0756-488578 |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli