TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Monduli anawatangazia wananchi wote wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kutuma maombi ya kazi kama zilivyotangazwa:-
1. Afisa Mtendaji Kijiji Daraja III - Nafasi 36
Kazi na Majukumu.
Kuwa mtendaji na mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na kamati zake.
Sifa: Mwombaji lazima awe na Elimu ya Kidato cha nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo:
Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo,
Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Umri: Mwombaji awe na umri kati ya miaka 18 – 40.
Ngazi ya Mshahara TGS B 1
2. Dereva Daraja II - Nafasi 6
Kazi na Majukumu.
Sifa: Mwombaji lazima awe na Elimu ya Kidato cha nne (IV) leseni ya udereva Daraja C na Cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II.
Umri: Mwombaji awe na umri kati ya miaka 18 – 40.
Ngazi ya Mshahara TGOS A 1
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 21/09/2017 saa 9:30 alasiri.
Maombi yote yatumwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya Monduli,
S.L.P. 1,
Monduli.
Monduli District Council
Sanduku la Posta: P.O BOX 1 Monduli
Namba ya simu: +255 - 27- 2538006
simu ya mkononi:
Barua Pepe: ded@mondulidc.go.tz
Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Monduli